Barua toka Jaramogi na Kenyatta
Wanauliza kama Kenya kuko sawa
Nikawajibu Kenya tuko na disaster
Watoto wetu wanazidi kuzikana
Na Tom Mboya ameshika tama
Alituacha kama angali kijana
Je, angekuwa mambo yangekua sawa?
Ndivyo alivyopanga maulana
Deni mlizowacha bado tunalipa (tunalipa)
Na tumekopa zingine China
Tukajenga reli pia barabara
Zilizobaki watu wakasanya
So tujiangalie (tujiangalie)
Tuko pabaya leo kuliko jana
Sikio la kufa halisikii dawa
Tuko kwa twitter tuna jibizana
Tujiangalie (tujiangalie)
Tuko pabaya leo kuliko jana
Tusipo ziba ufa tuta jenga kuta
Tusake zetu tungali vijana
Waumini kwa mathree na passie kwa bimmer
Kushoto fungu la kumi sadaka kulia
Ndio maana mbele ya kanisa mheshimiwa
Anakula sacramenti kabla ya raia
Siku za mwisho zime shawadia
Na revelation inatuambia
Hii generation inachoma picha
Ni generation yetu
So tujiangalie (tujiangalie)
Tuko pabaya leo kuliko jana
Sikio la kufa halisikii dawa
Tuko kwa twitter tuna jibizana
Tujiangalie (tujiangalie)
Tuko pabaya leo kuliko jana
Tusipo ziba ufa tuta jenga kuta
Tusake zetu tungali vijana
Michuki alisema, 'tufungeni mikanda'
Ona leo twavuna tulicho panda
Kura zetu zilitugawanya
Makabila na pesa pia tulimanga
So when you make your bed oh1
(You lie on it ohh!)
Usingizi gani tumelala?
Tuta jua hatujui
Vision 2030 itabaki ni story
Tujiangalie (tujiangalie)
Tuko pabaya leo kuliko jana
Sikio la kufa halisikii dawa
Tuko kwa twitter tuna jibizana
Tujiangalie (tujiangalie)
Tuko pabaya leo kuliko jana
Tusipo ziba ufa tuta jenga kuta
Tusake zetu tungali vijana
Nyashinski
Mdosi aliniambia freedom never comes for free
We vote tribe, ama real cash, ask Boni
Tuna roho mahali hamwezi Ita gsu plus doggy
World mzima twitter KOTndio first body
Burn picha si ni waafrika black coffee “Annan”
I’m richer than my neighbor but we both in the slum
If the rich always win why should the popular run?
Unless "democracy" ni word si usema only for fun
Tujiangalie (tujiangalieee)
Uh, na hii weekend tuko church tunauza sura kabisa
Post ya haga huenda poa sana na caption ya scripture
Kaa hiyo gospel pitisha bag ya sadaka kwa club
Yeeeah (tujiangalieee)
Uh, traffic madrug ubuy ndai, traffic mandai zinadrag
Ku admire mwizi amemake it, story za shamba wamegrab
Mkono nahonga imevaa bracelet ya colors za flag
Yeah!
1. Unapotandika kitanda chako, unakilalia